
LOML | Love Of My Life (77)

๐๐๐๐ (๐ณ๐๐๐ ๐๐ ๐๐ ๐๐๐๐) โฃ๏ธ:77
Walikumbatiana na alimuuliza โbibi yako yuko wapi?โ
Mtoto alisema โameenda mashineni hajarudi.โ
Pina alisema โooh amechelewa sana, haya kanisubiri nakuja.โ
Mtoto alienda, nikawa natazama ile nyumba namna ilivyo sijui hata mvua ikinyesha inakuaje huku. Ni nyumba chakavu sana.
Pina alisema โRicky Asante kwa kunifikisha hapa. Nakuombea heri kwa maisha yako. Tafadhali nakuomba sana Ricky. Ukae mbali na mimi, kaaa mbali na mimi kwasababu sihitaji rafiki haswa mume wa mtu.โ
Nilishtuka na kusema โPina, usinifanyie hivyo tafadhali.โ
Pina alitabasamu na kusema โUwe na usiku mwema Ricky, Mungu atakusaidia kila kitu kitaenda sawa. Niahidi tu utazingatia niliyosema.โ
Nilimtazama na kusema โNakuahidi lakiniโฆโ
Hakutaka hata kunijibu alianza kuondoka zake. Mimi nilibaki namtazama nikiita โPina!!!, Pina!!, tafadhali.โ
Hakutaka hata kunisikiliza, nilijikuta napata huzuni tena ndani ya moyo wangu kwanini Pina hataki Tena kuniona, ni kwanini?
Nilijisikia vibaya sana, nikiwa nimesimama natazama vile anaenda, anamchukua mtoto wake kwa upendo wanaingia ndani. Roho inaniuma sana. Alinitazama tu sasa sijui aliniona au ni nini, maana alinigeukia Mimi nikaita tena kwa huruma โPina nakuomba.โ
Aliingia ndani, ninakumbuka niliingia ndani ya gari Baada ya kusikia simu yangu ikiwa inaita sana. Alikuwa ni mke wangu. Simu Ina missed calls za kutosha. Nilichukia hata kuona jina pale eti wifey. Niliumia sana.
Baada ya hapo nikatoa sauti simu yangu kwanza. Sasa wakati nataka kuondoa gari tu. Niliona pale kwa Siti alikaa Pina kuna simu ndogo chakavu. Niliitazama na kusema โPina!!โ

