LOML | Love Of My Life (78)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:78
Wakati nataka kushuka nayo, nilipata wazo nijipigie nipate namba yake, haraka nikafanya hivyo na haikuwa na salio. Nilichoka, ilinibidi nibonyeze *106# kwa simu yake ili kujua namba yake na haraka nikaichukua na kuitunza kwangu.

Kisha nilishusha pumzi na kushuka. Nilitembea kuifuata ile nyumba. Baada ya hapo nilibisha hodi nikisema β€œPina tafadhali nakuomba.”

Ulipita muda kama dakika 3 mpaka tano hivi, Pina alitoka. Hakuwa na furaha kabisa macho yake yalikuwa Kama ametoka kulia hata nikamuuliza β€œulikuwa unalia Pina?”

Alinitazama na kuniuliza β€œunasemaje Ricky, tafadhali nakuomba usirudi tena hapa.”
Nilishusha pumzi na kusema β€œnimekuelewa ingawa siwezi kukuahidi hilo. Umesahau simu yako.”
Aliniambia kwa upole β€œooh nashukuru sana. Asante.”

Akawa anataka kuingia ndani na kisha nilishika mkono wake na kusema β€œPina marafiki tafadhali.”
Pina alinigeukia, akanitoa mkono wangu na Kisha aliniambia β€œHakuna thamani ya sukari kwa Supu, na hakuna thamani ya chumvi kwa chai.Δ°li supu iwe tamu inahitaji chumvi, na ili chai iwe chai inahitaji sukari.

Jua thamani yako na wapi unatakiwa kukaa. Usikubali kufit sehemu ambayo haustahili. Nakutakia usiku mzuri na Asante kWa leo.”

Nilimtazama tu, macho yake ni Kama na yeye ametoka kulia. Ila nitafanya nini hataki kuongea na Mimi. Wakati ndiyo naondoka, nilipishana na bibi hapa, ni wazi ni bibi yake na bibi alikuwa ananitazama sana lakini sikuweza kusema kitu.

Nilikuwa tu Nina mawazo tayari kichwani kwangu. Mpaka naingia kwa gari bibi bado ananitazama. Nilifunga vioo vizuri, nikashika simu yangu halafu ule uchafu wa Gabriella wote nikamtumia yeye mwenyewe.

Halafu nikazima simu yangu nilipo hakikisha zimemfikia.Nikawasha gari na kuanza safari ya kuondoka hapa nikiwa na maumivu sana moyoni kuhusu mambo yaliyo nitokea.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIOLOGY TEACHER FULL

UKO HOME NIJE FULL