LOML | Love Of My Life (79)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:79
Maneno ya Pina yalikuwa moyoni mwangu, nilikuwa Nakumbuka namna ana SalΔ± kwa utulivu na kumaanisha. Nilitamani Mungu anipe nguvu. Kusema ukweli wa moyoni sina nguvu ya kumkabili mke wangu. Matendo ya mke wangu ni makuu yanatisha sana.

Ninamuogopa sio kwasababu ni mjanja, ninamuogopa sababu ni kinyonga sio kinyonga, nyoka sio nyoka. Nikikumbuka nilimuita mbuni kumbe nilimuonea ndege yule mzuri kabisa. Huyu mwanamke sijui hata Bora ukutane na kitu gani kuliko huyu.

Moyo unauma, macho yanateseka, mwili unaumia, uwepo wake kwenye maisha yangu ni mwiba na kila nikikumbuka ni mke wangu, mke wangu wa ndoa inaniuma mara kumi elfu na elfu na elfu. Nateseka sana.

Sikutaka kurudi nyumbani, nilikuwa nina hasira. Ingawa niliambiwa nitulie na Pina. Niliambiwa nitumie hekima ila kiukweli sikuwa na hekima kwa wakati huu. Na pengine ningefanya tukio La kutisha kuliko matukio yote hapa duniani.

Ningemnyonga Max ndani ya gari yangu. Kitu pekee nilikuwa nawaza niende hotel nikalale huko na hapa najua wazi sasa mke wangu anajua nini amefanya na kwanini sipo nyumbani kama ana sherekea asherekee ila akae akijua mimi sio mbuzi wake wa kafara ni mwanaume wake.

Kipindi cha ndoa yangu, wakati tunawaza msimamizi na kunchagua Max mke wangu hakupinga hata alifurahia akisema β€œanafaa sana, mke wake ni mstaarabu bila Shaka atanifundisha vizuri kabisa.”

Wakati nahangaika kutafuta Mc mtandaoni tena Mc mzuri na yeye alisema wake ni moja ya vijana wanafanya vizuri sana hapa mjini. Ni Mc ambaye wanafanya naye kazΔ± sana kwa familia yake. Lakini sasa kwanini atembee naye na akubali kuwa Mc wa Sherehe ya ndoa yetu.

Tena walifanya hata nianze kumbuka ukaribu wao, namna wanapiga picha hata mimi bwana harusi sikuwa na picha nyingi na mke wangu Kama Mc na huyo Max sasa sijui wengine ambao mimi sijui.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIOLOGY TEACHER FULL

UKO HOME NIJE FULL

KIBOKO YANGU FULL