LOML | Love Of My Life (83)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:83
Nilikaa kitandani, nikawa nakumbuka vile namtoa out, vile nasikiliza mtoto anacheza tumboni, nakumbuka nilivyokuwa na hamu na mtoto azaliwe, vile nilikuwa nacheka na mke wangu nafanya kΔ±la kitu nyumba iwe na furaha, nafanya kila kitu nipate baraka za mke wangu.

Sasa hapa kuna baraka kweli, alikuwa anapata hata muda wa kuniombea kweli kwa mtindo huu. KΔ±la nikikumbuka mahusiano yangu na mtoto tumboni hoi, Yale mambo ya kizungu ya mke wangu, madeko yake ya kitandani, mahaba ya bafuni, kitandani, sebuleni, kazini kΔ±la nikiwa naye anaringa mume wangu wangu.

Nilijikuta nalia kwa nguvu nikisema β€œstupid, wewe ni mshenzi sana, hufai kabisa umechezea moyo na hisia zangu. Gabriella wewe ni shetani, jini wewe eeeenh, oooh!!, iiihiiiiii!!! Nalia kWa maumivuuu makali sana.

Sikumbuki kama nililala usiku huu, pengine ni ya kawaida ila kwa mwanamke wangu kufanya haya Nilitetemeka sikutamani tena kuendelea na hii ndoa sikuwa natamani. Nilijizuia sana nisimtafute kabisa Pina.

Na niliweza, unajua lakini usingizi ni usingizi mida ya saa 11. Usingizi ulinichukua, nilijisikia amani walau kupata usingizi huu. Niliamka nikaoga, niliagiza chakula lakini Baada ya kufika niliishia kukitazama tu.

Ile nawasha simu mpaka inaganda ni meseji ni kuita ni notification mbalimbali. Nimetafutwa sana na mke wangu, mama yangu, baba yangu, Giana, mama babuu, Willy, baba mkwe na mama mkwe nimetafutwa kupita kawaida.

Nilishusha pumzi, kisha nilisikia tena simu inaita, alikuwa mama yangu, nilipopokea tu nilisikia ana foka β€œhivi ndiyo nilivyo kulea?, kulala nje ya nyumba yako. Umewahi kuona baba yako analala nje bila sababu maalumu.

Kwanini unakuwa na tabia za ajabu namna hii. Mke wako ana kuhitaji, anataka mpaka kufa wewe haupo. Mwanaume wa namna gani wewe.”

Nilishusha pumzi, macho yangu yalizidi kuchoka. Hakuna mtu anajua mimi napitia nini, mara hii naonekana kama nataka kumuua mke wangu. Nilisema β€œmama nisikilize tafadhali.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata