
LOML | Love Of My Life (85)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:85
Hata Pina sikumtafuta, sikumfikiria kwasasa maana tena mambo yamekuwa mengi ndiyo yale alisema kuna muda unatamani kulia mambo tena yanakuzonga.
Nakumbuka nikiwa barabarani Shemeji yangu Giana alinituma ujumbe alisema βShemeji yangu, upo wapi?, huku hali sio nzuri, sijui mna pitia nini kwa ndoa yenu, mkeo alipoteza fahamu, mimba imeharibika tangu usiku tunahangaika wewe haupo kuna shida gani?β
Sikuweza hata kumjibu kwa maana najua huyu ni rafiki yake lazima tu anajua uchafu wa shoga yake. BaΕΔ± niliendelea kuendesha tu mpaka nikafika hospitali.
Niliuliza kuhusu mke wangu, vile naenda nakutana na baba na mama mkwe halafu kwa nyuma yao naona baba na mama yangu. Nilisalimia βShikamoni wazee wangu.β
Baba mkwe ndiye alijibu, huyu mama alinitazama kisha aliniuliza βUnataka kumuua binti yangu?.β
Nilishusha pumzi na kusema βnisamehe mama, haikuwa namna hiyo.β
Mama mkwe aliniambia βmwenzako anakutafuta hupokei simu na mwisho unazima kabisa. Ana hangaika kupambania uhai wa mtoto wenu na wake wewe haupo.
Nilikupa binti yangu ili umuue. Unafikiri kwamba una uwezo wa kumfanya hivi binti yangu. Na bahati yako binti yangu mzima, ungenielezea vizuri Rodricky, nakupenda najua nimepata kijana anajitambua kwa binti yangu Kumbe Hakuna kitu kabisa. Kama humpendi binti yangu si muache?β
Niliinamisha tu kichwa changu, baba mkwe alisema βmke wangu maneno makali hujui alipatwa na nini, sasa tusubiri mwingine aendelee vizuri tukae na watoto tuzungumze nao tuwaelekeze maisha tafadhali mke wangu.β