
LOML | Love Of My Life (88)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:88
Namna nalia labda hata baba alisema moyoni hili mbona dogo Kumbe mimi nimesema kwa kifupi kuna mengi. Baba alinikumbatia kWa upendo sana na kisha aliniacha nilie mpaka nilipotulia.
Nakumbuka baba yangu alisema maneno haya βKijana wangu Rodricky, wewe ni mtoto wangu. Nimekulea kwa upendo mwingi sana, nimekulea kwa namna nzuri sana.
Mwanangu kipenzi, wewe ndiyo tegemeo langu katika haya maisha. Kwenye hii dunia unatakiwa utambue kuwa kuna gharama kubwa sana kuwa mwanaume, tena sio mwanaume tu bali mwanaume anayejua maana ya maisha.
Wewe bado ni kijana, na mke wako pia bado ni binti. Kama mzazi sitaweza kukushauri tofauti na hapa ninavyo kushauri sasa. Ujana mambo mengi, ujana vitu vingi, ujana una mambo ya kila aina na mbaya zaidi tumepitia makuzi tofauti.
Wapo wenye wazazi lakini wanajilea wenyewe wazazi hawana muda, wapo wasio na wazazi na wana maadili mazuri sana ndiyo dunia.
Mungu aliona hili, akatufundisha kwenye maandiko yake kuwa Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo.
Maandiko hayo hayo yaliendelea kusema Basi, kimbia tamaa za ujana, na utafute kupata haki, imani, upendo na amani pamoja na wote wamwitao Bwana kwa moyo safi.Sitakuambia kuwa mke wako ni mbaya sana.
Ila nitakushauri ujaribu kumsaidia. Utakaa hapa unalia mtoto sio wako na hakuumi. Ila sisi familia, ndugu na jamaa wengine wote tunaumia, tuna guswa na kupoteza kwako kwasababu tunajua kuwa ni mke wako yule, ni mke wa ndoa wa kwako.
Kipenzi mwanangu, KITANDA hakizai haramu, hata kama angezaliwa wewe ungekataa bado watu wangekupongeza, unajua mtoto ni baraka, mtoto ni mafanikio.