LOML | Love Of My Life (89)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:89
Huwezi kujua mke wako maisha yake ya zamani pengine maisha yake hajamalizana nayo yanamuandama mpaka kwenye ndoa jaribu kukaa naye, au familia tukae pamoja na tuyaweke haya sawa.

Mungu hapendi watu kuachana, Mungu hapendi watu kupeana taraka. Kama kuna nafasi ndani ya moyo wako tafadhali tukae familia tumsaidie, tuwasaidie.

Lakini nitapenda kukusikia zaidi mwanangu, kwasasa huu sio muda wake, kamuone kwanza ujue anaendeleaje halafu mengine tutazungumza. Fanya kibinadamu, kama rafiki yako, ni mtu unalala naye kitandani.

Mwanangu, ndoa ni pamoja na kuwa na misuri imara, wewe ni mwanaume na mke yupo chini yako jaribu kumfanya mke, mpe mipango yako na mwambie nini unataka.

Ndoa miezi mitatu tu mwanangu, tafadhali ipeni muda tena Mungu azidi kuwatengeneza, mtazini hata lini kijana wangu?, unataka kuacha ndoa na uzini?. Najua unaumia, najua unateseka, najua una hangaika, mwanaume hakimbii nyumba yake yeye mwenye, mwanamke atakupanda kichwani.”

Nilikuwa namtazama baba yangu nalia machozi nikisema β€œbaba siweziii, siwezi baba yangu, naumia sana naumia.”
Baba alinikumbatia na kuniambia β€œjikaze mwanangu, nitaweka sawa hili jambo. Jikaze usilie rafiki yake yupo hapa sawa mimi naenda tutazungumza na tafadhali leo usilale nje ya nyumba yako. Wewe ni mwanaume, mwanaume.”
Nilikuwa namsikia baba yangu, nilikuwa najaribu nimuelewe lakini ni ngumu sana. Inaumiza.

Nakumbuka baba yangu, alinipigapiga mgongoni kwangu, halafu alianza kuondoka lakini walau nilikuwa na nafuu kifuani. Rafiki yake alifika na kisha aliniita β€œshem!!”

Nilimtazama kwa hasira na kumuuliza β€œulipanga kuniambia lini ushenzi na ujinga wa rafiki yako maana hutakiwi kuniambia hujui kuhusu tabia zake za ajabu.”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

KIAPO CHA MASIKINI FULL

UTAMU WA JAMILA FULL

SIMULIZI YA INGIZA FULL