LOML | Love Of My Life (91)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:91
π•Ύπ–Žπ–’π–šπ–‘π–Žπ–Ÿπ–Ž π•·π–Žπ–‡π–—π–†
Sikuwa najua hata ana maanisha nini, nilitikisa kichwa ili aendelee. Kisha alisema β€œajabu sana, wapo watu wengine wanapenda kuweka watu wanao wapenda, wanao waamini, wanao wafurahia kama akiba tu.

Wakifanya mambo yao wakimaliza wale wanaowapenda wanatumika kama kivuli kuziba na nafasi kipindi wao wanauhitaji huo. Ukitumika kama akiba, jitahidi sana kukubali hali hiyo, ili uoze, ukioza utanuka sana, harufu mbaya.

Yeye anaporudi kwako anakuta tayari umeoza, hufai, umebadilika tabia, hawezi kukugusa, hawezi kukusogelea kabisa.

Huelewi namanisha nini, badilika, mtu akikuumiza badilika, siku nyingine ajue kabisa kuwa wewe ni dhahabu anayo ichafu na inagoma kuchafuka.

Usikubali alichofanya jana afanye na leo, jana alikuacha ovyo leo akukute imara. Kuwa imara zaidi ya siku zote. Asante boss.”

Nilimshangaa sijui hata ana maanisha nini kusema kweli, wakati huu nilikuwa nachanganyikiwa tu. Nilishusha pumzi na kumtazama tu akiondoka. Nilimuacha huku natafakari kile alichokuwa ameniambia.

Niliendelea na safari niliingia mpaka ndani. Nilimuona mama yangu na baba wakizungumza. Mimi sikujali hata wanaongea kitu gani. Nilipitiliza tu kwa chumba cha mke wangu muuaji.

Nilipofika mlangoni, nilisimama kwa muda, nikunja ngumi zangu kwa maumivu sana, nilifuta machozi ili nikifika huko ndani nisilie, nisiwe mnyonge, niwe jasiri kama baba yangu alivyo nielekeza.

Niliingia ndani, Gabriella alikuwa kitandani ukimtazama amechoka kweli, amechoka haswa. Nilimtazama kwa hasira maana ndiyo namuona. Aliponiona alisema kwa huruma β€œmume wangu, Mume wangu, umefika mume wangu!!”

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

SHEM MI NATAKA FULL

KIBOKO YANGU FULL