
LOML | Love Of My Life (96)


LOML❣️96
nikiwa na simu yangu mkononi, mke wangu alipiga, nilisonya tu maana alifanya nikumbuke hadithi yake na huyo mwanaume wa madawa nikaona tu kama ananichezea akili, anajitetea sana, anatengeneza sana mambo ya kuleta huzuni na halafu hawezi kusimamia kitu anajitetea.
Mke wangu ni mtu anayependa ngono sana hatosheki labda au ni pepo, lakini hapa nisisingizie pepo zimetulia zake huko, ni yeye tu kitu kinacheza muda wote utulivu hakuna ni 0/0. Bora kuwa bila mwanamke kuliko mke ambaye nimeoa mimi.
Niliona tu ni bora nimpigie Pina, pengine atanipunguza mawazo na maneno yake. Lakini ninayo hofu kwasababu hakutaka tena kuwasiliana na mimi, hakutaka tena mazoea na mimi.Aliniambia wazi wala hakunificha kabisa. Nilipiga simu, iliita lakini haikupokelewa. Nilishusha pumzi tu na kusema moyoni “nitampigia baadaye, sina hata la kuongea naye sasa.”
Unajua una mtafuta mwanamke kutoka na heshima yake mpaka unatetemeka, nikaweka simu pembeni, ujumbe mwingime ukaingia. Nilijisemea kwa kulalamika “Gabriella!!, Gabriella!!, huwezi kupumzika wewe mwanamke?”
Nikavuta simu, hakuwa yeye ilikuwa ni namba hii ya Pina, na niliandika tu Pina. Nilishtuka kipofu amenitumiaje ujumbe. Hata nikasoma, ingawa haikuwa imekaa na maneno yote ila nilielewa, ilikuwa “npge tfdhali(nipigie tafadhali.”
Nilitabasamu na kusema “amewezaje, waooo, au kuna mtu amemuandikia?”
Haraka nilipiga, haikuchukua muda ilopokelewa na mimi nilisema “Hello Pina!!”
Kwa sauti nzuri, sauti ya utulivu, sauti ya mwanamke mwenye kujiheshimu na kujitambua, alijibu kwa kunishangaza “Hello, ni Rodricky right?.”