
LOML | Love Of My Life (97)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:97
πΎπππππππ π·ππππ
Nilishangaa, nilishindwa kujizuia kabisa kumuuliza swali hili βumejuaje ni mimi?β
Alinijibu kwa upole βhisia na kumbukumbu zangu. Nikimsikia mtu mara moja basi hata upite muda kiasi gani, nitafanya jitihada bila kukosea nitajua tu.β
Nilitabasamu na kusema βsafi sana, nimefurahu.β
Pina akaniuliza βunataka nini Rodricky?, umepata vipi namba yangu kwasababu sikumbuki kama nilikupatia.β
Nilianza kujiumauma, aliniendelea na kusema βalright, ni sawa haya unataka nini?, nilishasema kuwa sihitaji unitafute tena, sihitaji.β
Nilijibu kwa upole βnakuomba usikate simu Pina. Nisikilize huna haja ya kuwa na hasira. Mimi sio mtu mbaya, nilitaka kukujulia hali, na kuomba kukuona tena. Naomba nikuone tena, nahitaji kuzungumza na wewe tena, nakuomba.β
Pina alinijibu bila kuficha βhaiwezekani, hapana Ricky, sihitaji kukuona tena, naomba kaa mbali na mimi.β
Alikata simu, niliita ili hali najua amekata simu βPinaaaa!!, Pinaaaaa!!!, Pinaaaa!!!β
Nilitoa simu masikioni na kusema βni nini tena hiki, Mungu wangu. Pina hataki kuzungumza na mimi. Ooh.β
Nilijilaza pale kitandani, nilijisikia vibaya na ndani yangu nilidhamiria lazima nitaenda kumuona tu nyumbani kwao ni lazima.
Sikutoka hata chumbani kwangu, ninakumbuka nikiwa chumbani rafiki yangu Willy alipiga simu. Aliniambia βkaka unakwama wapi, wale wateja wamekuja wanahitaji mzigo wa kutosha na wewe huokoti simu, nimefika mpaka kazini kwako sikupati. Hakuna anayejua taarifa zako tunafanyaje kazi namna hii kaka?β
Nilivuta pumzi na kusema βnisamehe sana kaka, nisamehe sana. Unajua mke wangu alipata changamoto. Mimba ikaharibika basi ndiyo imekuwa hivyo hapa bado yupo hospitali.β