
LOML | Love Of My Life (99)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:99
Nilijiandaa, nilivaa nikapendeza. Wakati navaa pale, mke wangu alinitumia ujumbe βMume wangu, Goodmorning Handsome. Nipo hapa tena kukumbusha kuwa maisha yangu ni magumu sana kwasababu naishi nikijua nimekukosea. Naomba uje kuniona mume wangu.
Usiniache hapa hospitali mwenyewe. Nakuhitaji wewe, naomba mume wangu, nakuomba sana usinichukie kiasi cha kuniacha hapa, Please forgive me, Nakupenda sana Hubbyβ£οΈ.β
Nilisoma, unajua vile umetumiwa ujumbe halafu wewe pamoja na maneno ya mashiko aliyokuandikia unaona ni kejeli tu. Sasa ndiyo nilivyokuwa namuona huyu mwanamke kwangu.
Sasa akatuma na wimbo wa Bryan Adam unaitwa Please Forgive me. Niliplay nikawa nasikiliza pale, nakumbuka tu baadhi ya mistari ya kiitikio cha wimbo huu. Ni wimbo mzuri sana kwa wapenzi wa kweli, wale ambao amefanya kosa dogo tu sio kama huyu wangu, ina maneno mazuri ukijua wimbo umetoka kwa mtu anaye maanisha sio huyu wangu.
Kile kiitikio kinasema βPlease forgive me, I know not what I do
Please forgive me, I canβt stop loving you
Donβt deny me this pain Iβm going through
Please forgive me, if I need you like I do
Please believe me, every word I say is true
Please forgive me, I canβt stop loving you.β
Nilitoa wimbo wenyewe, na kisha nilisema βshikilia msimamo wako. Wewe ni mwanaume usiyumbe.β
Nilibeba bag yangu ya kazini na kisha nilianza kutoka zangu. Nilikutana na mama Babuu. Alinisalimia na nilimjibu, aliniambia βboss kama unaenda hospitali tunaweza kuongozana tafadhali?β