LOML | Love Of My Life (258) MWISHO

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️: 259
Yapo yanayomwongezea ujuzi, uwepesi na umahiri.
Ninachojaribu kusema ni ubora wa mchezaji hautokani na uwezo wake wa kucheza au kushindana bali maandalizi yake na mazoezi yake. Kadhalika katika mambo ya rohoni. Maandalizi ni muhimu mno mno mno.
Usisubiri upate shida ndo uombe.


Yapo maombi kwa kusudi la kupata majibu ya mambo mbali mbali maishani alafu yapo yale ambayo ni maandalizi na mazoezi hasa yale ambayo unalazimika kila siku kuamka kuomba.

Unapotegea maombi yako binafsi au yale ya kanisani kwenu au kikundi ulichopo unajitegea mwenyewe kwenye maandalizi na mazoezi yako ya kiroho.
Kadhalika usomaji wa neno na kufunga.

Vyote hivi ni mazoezi ya kiroho yanayomwimarisha na kumtia nguvu mtu wa ndani ili siku ya mechi (changamoto, taabu, shida, uhitaji) uwe upo vizuri kukabiliana.
Wengi tunafeli siku ya dhiki maana nguvu zetu ni kidogo.

Hatujajijengea nidhamu ya kuomba, kusoma neno, kuhudhuria ibada, kufunga nk ambayo itamwimarisha na kumwandaa mtu wetu wa ndani kwa ajili ya siku ya uovu na vita.

Kama mazoezi yalivyo ya muhimu kwa ajili ya kumwandaa mwanamichezo hodari, mahiri, mwenye ujuzi, pumzi na nguvu, kadhalika mazoezi ya kiroho ni muhimu mno kwa ajili ya kumwandaa wewe mwenye nguvu za kiroho, pumzi ya kiroho, umahiri na uweledi wa kiroho.
Acha kuendelea kupuuzia mazoezi ya kiroho.

Itakugharimu siku ya vita.
Kumbuka: Jasho jingi mazoezini, damu chache vitani. Jasho kidogo mazoezini, damu nyingi vitani.
β€œKwa maana kujizoeza kupata nguvu za mwili kwafaa kidogo, lakini utauwa hufaa kwa mambo yote; yaani, unayo ahadi ya uzima wa sasa, na ya ule utakaokuwapo baadaye.” (1 Ti.4:8).

Kwa wale waliyoamua kumfanya Yesu Bwana na Mwokozi wa maisha yao hakuna laana na baraka bali kuna baraka tu. Kwa hiyo mtu wa Mungu uwe unayaangalia maandiko ya Agano la Kale na kuyasoma na kuyaelewa katika muktadha sahihi wa Agano Jipya la Neema.

Tunapokosea hatujiletei laana bali tunajiletea kurudiwa na Bwana maana Mungu kwetu ni Baba na sio Baba Aliye mwepesi wa hasira yaani tukikosea tu anatulaani. Atatukemea na kuturudi ndiyo lakini kutulaani hapana maana ameshatubariki kwa baraka zote za rohoni katika ulimwengu wa roho ndani ya Kristo Yesu sio kwa sababu ya chochote tulichofanya bali kwa sababu ya kile Yesu alifanya kwa ajili yetu pale msalabani.


Yeye asiyejua dhambi alifanywa dhambi kwa ajili yetu ili sisi tuwe haki ya Mungu katika Kristo Yesu. Kristo alitukomboa toka katika laana ya Torati maana alifanyika laana kwa ajili yetu au kwa maneno mengine badala yetu, maana imeandikwa amelaaniwa kila mmoja aangikwaye juu ya mti ili baraka ya Ibrahimu itufikilie sisi mataifa kupitia Kristo Yesu. Laana zimeshachukuliwa na Yesu kwa hiyo haiwezekani wewe uliye katika Yesu ulaaniwe.


Acha kuwaza mauti na laana anza kuwaza uzima na baraka vilivyo fungu lako katika Kristo Yesu. Roho hushuhudia pamoja na roho zetu kuwa sisi ni wana wa Mungu na kama ni wana basi tu warithi turithio pamoja na Kristo. Kama tu warithi turithio pamoja na Kristo, kama Yesu hawezi rithi laana mimi siwezi kurithi laana. Kama Yesu ni mrithi wa Baraka za Baba Yake mimi pia ni mrithi wa Baraka.

Kama Sira 25:4 inavyosema Ni jambo zuri mno kwa mzee mwenye mvi kuamua vema, na mwenye umri mkubwa kujua namna ya kushauri! Natamani sana tungekuwa na wazee wengi Kama baba yangu. Ambaye ndiyo ninavyojiona mimi sasa.

Maisha yangu yamebadilika baada ya kukutana na LOML Vipi wewe umekutana naye au bado?. Usifanye haraka kuharakishia mahusiano na usibebe moyoni mahusiano yaliyo kuumiza jana. Lia kidogo songa mbele na ufurahie maisha yako. Mimi na familia yangu tumefuta yote ya zamani na tunaishi vizuri sana. Wazazi wangu ni wazee sana sasa, ni wazee lakini Tunamshukuru Mungu kwa baraka ya uhai wao na tunafurahia uwepo wao tukiwa na furaha sana.

π‘΄π’˜π’Šπ’”π’‰π’ π’˜π’‚ π’”π’Šπ’Žπ’–π’π’Šπ’›π’Š π’šπ’‚π’π’ˆπ’– π’šπ’‚ 𝑳𝑢𝑴𝑳❣️, π’π’Šπ’”π’‚π’Žπ’†π’‰π’† 𝒔𝒂𝒏𝒂 π’Œπ’‚π’Žπ’‚ π’”π’Šπ’‹π’‚π’‡π’Šπ’Œπ’Šπ’‚ π’Žπ’‚π’•π’‚π’Žπ’‚π’π’Šπ’ π’šπ’‚π’Œπ’.

ASANTEE

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

BIKIRA YA BIBI HARUSI FULL

SIMULIZI YA INGIZA FULL

BIOLOGY TEACHER FULL