SEASON 2: LOML | Love Of My Life (68)

π‹πŽπŒπ‹ (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 π’Žπ’š π’π’Šπ’‡π’†) ❣️:68
β€œUsiniache hapa Pina nakuomba, nahitaji mtu wa kuzungumza naye walau nijisikie mwepesi. Walau aniambie kila kitu kitakuwa sawa, aniambie nitakuwa sawa, mimi nitakupeleka popote, Pina unaweza kubaki na mimi kwa muda hata kidogo tu, hata kidogo.”

Niliona macho ya msichana huyu yanajaaa hisia za maumivu, sasa yeye haoni, ila mimi naona Kwahiyo nina mtazama na vile na Mimi nina maumivu makali sana moyoni mwanangu hata kuelezea haya maumivu ni ngumu sana.

Msichana huyu alipiga hatua chache kunisogelea, halafu aliinua mkono wake mmoja na kuanza kunipapasa usoni, alinipapasa kwa namna ambayo mimi vile ananigusa ninasikia amani sana. Halafu alinikumbatia, sijui nikuambie nini.

Sikuwahi kuhisi, sikuwahi kujua, kuwa kwenye haya maisha yangu, siku moja kumbato tu kutoka kwa msichana wa aina ya Pina litakuwa dawa kwangu. Nimetoka kWa familia nzuri, mimi nyumbani kwetu kila kitu tunatatua kwa pesa.

Kumbe kuna mambo pesa haiwezi kufanya. Pesa haiwezi kukupa furaha kama hauna amani. Nilijikuta nasema kwa upole β€œnashukuru sana Pina, Nashukuru sana Pina.”

Mimi ni mwanaume, Tena mwanaume ambaye ukiniona unasema kabisa kaka yule ni mtu makini sana, hana masihara muda wote yupo serious, muda mwingi yupo makini sana lakini wakati huu sikuweza, nilikuwa nalia, nilikuwa naumia, nilikuwa sijisikii vizuri tena, sikuweza kuyazuia machozi yanayotoka kwenye moyo wangu uliojaa huruma ya kutosha sikuweza.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata

TOBO LA PANYA FULL

UTAMU WA JAMILA FULL

UKO HOME NIJE FULL

CHAGUO LA MOYO FULL