
SEASON 3: LOML | Love Of My Life (117)


ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:117
Nilisoma, nilisoma kwa kumuhurumia lakini Sikutaka kumzingatia, Mara uliingia mwingine βnipo nyumbani mume wangu, usinitelekeze kama hunijui. Naomba tuzungumze mume wangu. Nakuomba uje kunichukua.β
Nilisoma tu na kuona nachanganyikiwa. Niliamua kumpigia simu rafiki yangu Willy. Willy alipokea simu yangu na kusema βkaka Upo wapi?β
Nilimwambia kwa upole βUpo wapi?, leo nataka kunywa kidogo.β
Willy alicheka mna Kisha aliniuliza βkwema?β
Nilimwambia kwa kusema βhata sielewi kabisa, nataka tuonane tu nipunguze mawazo.β
Willy aliniambia βnakufuata hapo sio muda. Jiandae.β
Nilivuta pumzi na kusema βfanya haraka.β
Akaniambia kwa upole βnaacha garΔ± nakuja na pikipiki.β
Nilimtazama na kusema βni sawa, Hakuna shida.β
Nilitoka nje mpaka kwa gari yangu, nilikaa nimejiinamia tu. Kiukweli sina raha kabisa, maisha yangu yote naona Hakuna raha naipata. Nilisubiri kwa muda, na Kisha rafiki yangu alifika.
Nilimfungulia mlango wa gari na akaingia, aliponiona tu, nilijikuta machozi yananitoka sana. Alinikumbatia kwa nguvu, akinipigapiga mgongoni na mimi nikiongea kwa uchungu βnajikaza kaka nashindwa nashindwa kabisa.β
Willy alinituliza sana, Kisha aliondoa gari. Alinipeleka mpaka ufukweni. Nakumbuka sana. Tulishuka na hata nikamuuliza βumenileta hapa kufanya nini kaka?, nataka kulewa.β
Alinitazama na kuniambia βwewe ni ndugu yangu, siwezi kukupeleka kulewa kama sehemu ya kΓΌpΓΌnguza maumivu yako. Kaa hapa, Ila unavyotaka ukimaliza nakuomba niambie nini kinasumbua.β
Nilimtazama na kusema kwa upole βmke wangu kaka, mke wangu.β
Willy alishangaa na kuniuliza βmke wako?, mbona mlikuwa na furaha sana leo pale ndani.β