
SEASON 5: LOML | Love Of My Life (207)

ππππ (π³πππ ππ ππ ππππ) β£οΈ:207
Baba alitabasamu tu. Nilimshika mkono mpaka chumbani kwangu. Nilipofika huko nilimshika vizuri na kumuuliza βUpo sawa mpenzi ?β
Aliniambia kwa upole βNipo sawa mpenzi. Ninakuacha uwe huru na baba wakati mimi namalizia uzingizi wangu Kisha mkimaliza nirudi nyumbani kesho nitakuja kukuona tena si ni sawa?β
Nilimtazama na kusema βnilijua utalala eti?β
Alitabasamu na kusema βsio leo mpenzi ungekuwa unaumwa bado sawa.β
Nilicheka nikisema βhuoni naumwa sana ujue Pina wangu.β
Tulijikuta tunacheka tu.Kisha mimi nilitoka na kumuacha Pina kitandani.
Baba yangu aliponiona natabasamu na yeye alitabasamu na kusema βanaonekana ni binti mzuri sana. Ana heshima na upendo sana. Sijui kwanini Ila Nina furaha sana nikikuona na huyu binti. Mtafika mbali sana.β
Nilitabasamu na kusema βbaba Nina furaha sana. Hata sijui kwanini nilikuwa nachelewa kuwa naye. Yeye ni kila kitu nahitaji kwenye maisha yangu.β
Baba alicheka kidogo na kusema βndiyo ukamuoa tena kikokoteo.β
Nilicheka na kusema βbaba una nini lakini?β
Baba alisema βsasa tuseme nini na wakati sijui yeye ndiyo mwanaume au mwanamke. Yule binti ni mchawi nashukuru Mungu hajakuua mwanangu.β
Nilishusha pumzi, baba alisema βnilikuja kukuona na nafurahi kuona unaendelea vizuri. Lakini pia namba ya mwanasheria mzuri wa mambo ya taraka huyu hapa mwanangu.
Atakusidia kΔ±la kiti nishazungumza naye unajua cha kufanya. zaidi ya hapo ni kanisani na ukweli sasa ndiyo utakuweka huru. Muhimu unajiondoa kwa kifungo hiki. Nadhani unanielewa kijana wangu.β
Nilimkumbatia baba na kusema βbaba wewe ndiyo kila kitu. Nafurahia sana unavyo niunga mkono. Natumaini siku moja mama atanielewa na tutakuwa na furaha sana.β

