
LOML | Love Of My Life (167)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:167
Niliita “Pina upo sawa?”
Pina alisogea kidogo, kisha alinifuata mpaka nilipo na alisema kwa upole “nisamehe sana kama nimekosea kwa mama na mkeo. Nilitaka ujisikie vizuri, nilitaka nimgawie mkeo maumivu yako, sikutaka akuumize tena na mimi nikiwepo. Nisamehe sana.”
Willy alishangaa, nilimtazama Willy na kusema “Kaka unaweza kutuacha tafadhali.”
Willy alinitazama na kusema “bila shaka kaka.”
Aliinuka na kutoka zake.
Alipotoka nilipambana nikakaa, na yeye alinisaidia na kusema “Hey my girl, napenda unavyonitetea, unavyo nipambania. Kusema kweli peke yangu bila wewe siwezi.
Umenipa nguvu ya kupambana, na kujiona nina thamani kubwa. Mimi najua uliyosema yote una maanisha Pina. Ina maana ulikuwa unatania kuwa unanipenda sana, utaniheshimu na kunijali sana.”
Pina alitabasamu na kisha alisema “Ricky pleaseee!!”
Nilimvuta akae karibu yangu na nilimkumbatia na kusema “Pleaseeeee!!, Pleaseeeeee!!, nakupenda.”
Akaniambia kwa upole “Wapo sahihi, sikustahili, siendani na wewe, sivutii, sioni, maskini na bado ninaye mtoto, zaidi ya hayo yote nina maumivu makali.”
Nilisema kwa upole “Pina mimi ndiyo sikustahili, siendani na wewe, sivutii, sioni na mimi ndiyo maskini kwasababu ni
Mjinga na mpumbavu niliacha mjinga kama yule atawale hisia zangu.”

