LOML | Love Of My Life (193)

𝐋𝐎𝐌𝐋 (𝑳𝒐𝒗𝒆 𝒐𝒇 𝒎𝒚 𝒍𝒊𝒇𝒆) ❣️:193
Baba alisema “nisamehe mwanangu tangu jana uniambie namuwaza huyu binti Gabby sijui umewezaje kuishi naye Kumbe ni shetani namna hii. Naomba unataniambia ratiba zako lazıma tushughilikie hili. Kama hawakuelewi nakuja.”

Nilimzuia baba yangu nikisema “hapana baba narudi.”
Başı muda wa saa 6 ilikuwa hivyo, niliruhusiwa. Nakumbuka nikiwa njiani nilimpigia Pina na kumuelezea kuwa baadaye aje nyumbani nitaagiza dereva amfuate. Pina alifurahi sana akisema “nimefurahi unaendelea vizuri. Nitakuja kukuona. Nitakuwa nasubiri dereva.”

Nilitabasamu nikisema “nashukuru sana dokta wangu. Nakupenda sana Pina, Mrembo wangu.”
Alicheka na kusema “yaani wewe, nakuja kukuona. Nakupenda kuliko unavyo nipenda.”

Nilitabasamu tu, na Kisha nilisema “Nina zawadi yako.”
Akaniuliza kWa kudeka “Umeanza hivyo, ipi tena?”
Nilitabasamu na kusema “ndiyo mpaka ukija sasa.”
Alicheka tu akisema “we haya tu, Nina hamu na hiyo zawadi.”

Baada ya kukata niliomba dereva anipitishe sehemu nzuri wanayouza vitu vya hospitali. Başı hapo nilichagua fimbo nzuri sana ya kumsaidia kutembea na Baada ya hapo niliingia ndani ya gari na kuelekea ofisini kidogo kuna vitu sikuacha sawa.

Share kwa ndugu na marafiki

WhatsApp
Facebook
Twitter

Chagua kipande kinachofuata